NAFUNGA MWAKA NA WASHAMBULIAJI WA KIUCHUMI (ECONOMIC HIT MEN)
"Ecuador ni mfano halisi wa nchi ulimwenguni ambazo sisi washambuliaji wa siri wa kiuchumi tumezitia katika mbinyo wa kiuchumi. Kwa kila dola 100 inayozalishwa kutoka katika mafuta ghafi yanayochimbwa kutoka misitu ya Ecuador, makampuni yetu (ya Kimarekani) yanapokea dola 75. Dola 25 zilizobaki, robotatu yake inakwenda kulipa madeni (kwa Wamarekani na mashirika ya fedha ya kimataifa). Sehemu kubwa (ya kile kidogo kinachosalia) inakwenda kugharamia manunuzi y kijeshi na matumizi ya kawaida ya serikali (ya Ecuador).
Takribani dola mbili na nusu tu ndio hubaki kwa ajili ya afya, elimu na miradi inayolenga kuwakwamua masikini.
Hivyobasi, katika kila dola 100 zinazozalishwa kwenye mafuta, chini ya dola tatu ndio huenda kwa masikini ambao kimsingi ndio wanaozihitaji sana: wale ambao maisha yao yameathiriwa sana na visima, uchimbaji na mabomba na ambao hufa kutokana na kukosa chakula cha uhakika a maji salama.
Watu wote hawa-mamilioni ya WaEcuador na mabilioni ya masikini duniani ni magaidi watarajiwa! Si kwa sababu wanaamini katika Ukomunisti** au wamezaliwa na uovu-la hasha. Ni kwa sababu WAMECHOKA".
Nukuu hii (tafsiri ni yangu) nimeitoa kwnye kitabu cha Confessions of an Economic Hitman (uk xx) cha John Perkins. Mwandishi ambaye kwa miaka mingi alitumiwa kama shushushu kwenye kampuni la kimarekani anasimulia jnsi washambuliaji wa Kiuchumi(Ecnomic Hitmen) wanavyotumiwa na makampuni makubwa yakimarekani kuzitia katik mbinyo wa kiuchumi nchi masikini na kama ilivyo kwa chatu akiminyavyo kitoweo chake, kuziweka kwenye himaya ya ubeberu wa Marekani na nchi nyingine za kimagharibi.
**Mwandishi anaufungamanisha ukomunisti na ugaid kwa sababu wakati wa vita baridi, wakomunisti waliitwa hivyo na mabeberu.
Ninaendelea kukisoma kitabu hiki katika kuufunga mwaka. Ni kitabu murua cha toba. Swali ni je, katika kipindi hiki cha ugunduzi wa gesi na dalili za ugunduzi wa mafuta, tumejifunza vya kutosha kutoka kwa wenzetu?

0 comments:
Post a Comment