Video Queen, Agness Gerald.
KATIKA ulimwengu wa sanaa ikiwemo ya muziki na
filamu, mashabiki wamezoea kuwaita mastaa f’lani kwa majina wanayotumia
katika kazi zao ambapo majina hayo yamekuwa maarufu na yale halisi
waliyopewa na wazazi wao yakisahaulika kabisa.
Staa wa filamu Bongo, Blandina Chagula.
Katika makala haya tutakuletea orodha ya mastaa ambao majina
waliyotumia kwenye nyimbo au filamu yamekuwa ni maarufu kama ndiyo
halisi wakati wana majina waliyopewa na wazazi wao.MASOGANGE Huyu ni
Video Queen wa video za wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva, jina halisi
alilopewa na wazazi wake ni Agness Gerald.
Jina la Masogange lilikuja baada ya kushiriki kwenye video ya Wimbo
wa Masogange ambao umeimbwa na Mbongo Fleva, Abednego Damian ‘Belle 9’
hivyo kuanzia hapo limekuwa ni jina maarufu ambalo mashabiki
wameshalizoea kama lake halisi. Johari Huyu ni staa wa filamu Bongo,
jina lake halisi ni Blandina Chagula.
Johari lilikuwa maarufu baada ya kucheza filamu iliyokwenda kwa jina
la Johari ambayo ndiyo imemfanya ajulikane ndani na nje ya nchi ya
Tanzania. Binti Kiziwi Mwanadada huyu ambaye ni Video Queen jina lake
halisi ni Sandra Khan kwa sasa anatumikia kifungo nchini China kutokana
na kukutwa na madawa ya kulevya jina hili la Binti Kiziwi alilipata
baada ya kushiriki kwenye wimbo wa msanii wa Bongo Fleva, Z-Anto
unaojulikana kwa jina la Binti Kiziwi.
Video hii ambayo ndiyo chimbuko la jina la Binti Kiziwi ndiyo
ilimtambulisha mwanadada huyu kwa mashabiki na jina kuwa maarufu mpaka
leo.
Shumileta Ni staa wa filamu Bongo Movies ambaye kwa sasa anaishi
nchini India, jina alilopewa na wazazi wake ni Jennifer Mwaipaja.Jina la
Shumileta alilipata baada ya kucheza filamu iliyojulikana kwa jina la
Shumileta akiwa kama mhusika mkuu na hapo ndipo jina hilo lilianza kuwa
maarufu mpaka sasa wengi wanamfahamu kwa jina hilo.


0 comments:
Post a Comment