Leo
nimetembelea eneo la Stockyard katika soko kuu la Majengo nikiwa na
Meneja wa NSSF wa mkoa wa Dodoma Bi Rehema H. Chuma ambapo tumeangalia
eneo la stockyard ambalo halina paa na hivyo mazao mengi kuharibika kwa
jua kali na mvua.Eneo hili limekuwa kero kubwa kwa wafanyabiashara
wadogo wadogo wa matunda na mboga mboga tangu uanzishwaji wa soko hili
mwaka 1996.
NSSF wamekubali kutoa semina kwa wafanyabiashara wa masoko yote ya Jimbo la Dodoma mjini itakayofanyika siku ya Jumatano tarehe 11.11.2015. Baada ya semina watawasajili wafanyabiashara kuwa wanachama wa mfuko.Wanachama hawa watapata fursa ya kupata matibabu na mikopo kupitia michango yao ya kila mwezi.
NSSF wamelipokea ombi letu la kuweka paa katika eneo la soko ili kuwatengenezea kivuli wafanyabiashara wa soko la Majengo na kuahidi kulifanyia kazi pale bajeti yao itakaporuhusu.#DodomaMpya#

0 comments:
Post a Comment