MAMBO
mengine ni ya kuyasikia yakiwatokea wenzako na usiombe yakakukuta kama
ilivyomtokea msichana huyu ambaye hakufahamika jina lake mara moja baada
ya kuchukua kipigo ‘hevi’ ambacho nusura apoteze maisha yake, maeneo ya
Sinza Afrikasana, juzi Jumatatu.
Mashuhuda
wa tukio hilo wanasema, binti huyo akiwa na mwanaume mmoja, walionekana
wakitoka katika baa iitwayo Kona, wakiongozana hadi kwenye baa nyingine
iliyo maeneo ya Afrikasana ambako waliendelea na kinywaji.
“Yule
msichana ni mmoja wa wanaojiuza pale Kona, nadhani walikuwa na
makubaliano ambayo wamefikia, maana walikuwa wakinywa kwa raha zao,
ghafla tukasikia wanaanza kuzozana, jamaa alikuwa anataka waondoke,
bibie akawa analeta longolongo,” alisema dada mmoja aliyekuwa eneo la
tukio.
Inadaiwa
kuwa dada huyo alianza kupiga yowe akitaka apewe kiasi cha shilingi
30,000, ndipo mwanaume huyo ambaye alitoweka haraka, alipoamua kumpa
kipigo kikali kiasi cha kumpasua kichwani na kumsababishia maumivu
makali.
Baada
ya kupokea kipigo hicho, baadhi ya wahuni walifika eneo hilo na
kuendelea kumfanyia vitendo vya kidhalilishaji hadi akina mama wa eneo
hilo walipoamua kumhifadhi kwa kumfunika kanga, lakini katika hali ya
kushangaza, msichana huyo alipitiwa na usingizi mzito.Kuona hivyo,
majirani hao waliamua kumpeleka polisi ambako hata hivyo alifukuzwa kwa
kile kilichodaiwa kuwa ni mlevi.
0 comments:
Post a Comment