,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Sunday, July 26, 2015


NIMEHEMEWA! Wanawake wa UWT/CCM Mkoa wa Tanga wameonyesha imani kubwa sana sana kwangu kwa kunipa kura 786 kati ya kura 793 ili kuwawakilisha Bungeni 2015 - 2020.


Ninapenda kutumia ukurasa huu leo KUWASHUKURU kwa dhati wana UWT wa Wilaya zote za Mkoa wa Tanga kuanzia Kilindi, Handeni, Lushoto, Korogwe Vijijini, Korogwe Mji, Muheza, Pangani, Mkinga na Tanga Mjini. NINA DENI KUBWA SANA KWAO. Ninawaahidi Utumishi uliotukuka ktk kusukuma mbele maendeleo ya wanawake na watoto wa Mkoa wa Tanga. Narudia kusema tena "NIMEHEMEWA". Alhamdulillah. Sasa ni Mbele kwa Mbele ktk kutafuta ushindi wa CCM kwa nafasi ya Rais, Wabunge na Madiwani 25 Oct 2015.
-----
Matokeo UWT mkoa wa Tanga

Kura zilizopigwa 797. Kura zilizoharibika 4. Kura Halali 793.
1. Ummy Mwalimu 786 (99.1% ya kura zote)
2. Sharifa Abebe 431
3. Aisha Kigoda 118
4. Saumu Bendera 91
5. Sophia Mhilu 84
6. Laicky Gugu 52
7. Josephine Mgaza 8
8. Asia Kalage 7
9. Farida Mashaka 7
10. Angella Mganga 3


Hivyo waliopitishwa nafasi ya Ubunge Viti Maalum Wanawake/CCM Mkoa wa Tanga ni Ummy Mwalimu na Sharifa Abebe.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi