Los Angeles, Marekani
MWANADADA mwenye mikogo mingi, Kim Kardashian, amefunguka rasmi kuwa anatarajia kujifungua mtoto wa kiume.Kim, alifunguka hayo siku ya Baba Duniani ambayo iliadhimishwa wikiendi iliyopita na kumaliza tetesi zilizokuwa zimezagaa mtaani kuwa ni mjamzito.

Mama huyo mwenye umri wa miaka 34, alitumia mtandao wa Twitter, kumshukuru mume wake Kanye West, kwa malezi bora anayompa mwanaye wa kwanza anayejulikana kwa jina la North.
“Wewe ni baba mzuri kwa North na utakuwa baba mzuri pia kwa mtoto wetu wa kiume ajaye.”
Mara baada ya taarifa hiyo kutoka mitandao mbalimbali ilianza kuifuatilia na kila sehemu ikawa ikiandika kwa mtazamo tofauti.
Pamoja ya kuwa na ujauzito huo muendeshaji huyo wa kipindi cha Keeping Up with the Kardashians, juzi aliibuka kwenye maonyesho ya mavazi ya CFDA Fashion yaliyofanyika jijini New York Marekani.
Ni wiki moja tu imepita tangu North aliposherehekea kumbukumbu yake ya kutimiza miaka miwili jijini California, Marakeni.

0 comments:
Post a Comment