KAJALA Masanja ambaye ana bifu na aliyekuwa shosti wake mkubwa, Wema Sepetu ‘Madam’ amedaiwa kumpa rafiki yake huyo wa zamani ujumbe unaoashiria upendo kwa kuvaa gauni lenye maandishi yaliyosomeka “Love will save us” yakimaanisha upendo utatuokoa.
Baada ya mwandishi wetu kushuhudia ujumbe huo mgongoni mwa Kajala huku marafiki zake wakidai ni maalum kwa Wema ambaye amekuwa mzito kusamehe ugomvi wao, alimuuliza kama amemlenga Wema au ni vazi tu alivaa?
“Jamani mimi nimevaa tu, sikumkusudia mtu,” alisema Kajala.Wema na Kajala wamekuwa kwenye bifu la kuchukuliana bwana na bado hawajafikia muafaka.
0 comments:
Post a Comment