Posted by Williammalecela.com on Monday, May 25, 2015
Mkurugenzi wa Endless Fame, Wema Isaac Sepetu akiwa ameshika tuzo yake.
MKURUGENZI
wa Endless Fame, Wema Isaac Sepetu, juzikati alionesha maajabu ya aina
yake baada ya kuwagaragaza waigizaji wenzake Jacqueline Wolper,
Elizabeht Michael ‘Lulu’, na Riyama Ally katika kinyang’anyiro cha Tuzo
za Watu.
Wadau
mbalimbali waliohuzuria wakufuatilia hafla hiyo ya utoaji tuzo. Tukio
hilo lilijiri usiku wa kuamkia Mei, 23 mwaka huu katika Hoteli ya Hyatt
Regency iliyopo Posta jijini Dar es Salaam.Wema aliibuka kinara na
kuwafanya baadhi ya mashabiki wake walipuke kwa shangwe huku Wolper,
Lulu na Riyama wakibaki kimya.
0 comments:
Post a Comment