
Lori
lililosababisha ajali na kuua mwanafunzi na kusababisha wanafunzi wa
shule za msingi Tunduma kulala barabarani wakishinikiza kuwekwa kwa
matuta.

Baadhi
ya wanafunzi wa shule za Msingi Umoja,Mlimani na Tunduma za mjini
Tunduma wakiandamana kushinikiza kuwekwa matuta kwenye inayoelekea
Sumbawanga kutokana na ajali za mara kwa mara zinazosababishwa na mwendo
kasi wa madereva.
Lori linaloonekana pembeni limepinduka, limesababisha ajali na kuua mwanafunzi.
Lori linaloonekana pembeni limepinduka, limesababisha ajali na kuua mwanafunzi.


Askari
wa usalama Barabarani mjini Tunduma akipewa maelezo ya hali ya mtoto
aliyejeruhiwa katika ajali hiyo Jackson Sichalwe(7) kutoka kwa baba yake
Mzazi Norbert Siichalwe,Mtoto Jackson amelazwa katika hospitali ya
serikali mjini Tunduma baada ya kugongwa na gari ambalo pia
lilisababisha kifo cha Emmanuel Sichalwe mwanafunzi wa shule ya msingi
Umoja ya mjini Tunduma

Mamia ya wakazi wa mji mdogo wa Tunduma wakiwa katika mkusanyiko kufuatia taharukii iliyoibuka mjini i

Diwani
wa Kata ya Tunduma Frank Mwakajoka akizungumza na wanaanchi baada ya
kutokea tafrani iliyosababisha wanafunzi wafunge barabara kwa
kushinikiza kuwekwa matuta.Picha na Rashid Mkwinda
SAUTI zilizochanganyika na hisia na majonzi kutoka kwa wanafunzi wa
shule tatu za Msingi, Umoja, Mlimani na Tunduma zilisikika hewani na
kutoa ujumbe ulioashiria kupata ufumbuzi wa tatizo la ajali za mara kwa
mara katika barabara kuu iendayo Sumbawanga kutokea mjini Tunduma.
Ijapokuwa zilikuwa ni sauti za watoto, zilibeba ujumbe mzito wenye
shinikizo la uchungu uliofuatia kufariki kwa mtoto mwenzao Emmanuel
Sichalwe (7) ambaye aligongwa na lori na kufariki hapo hapo baada ya
kukanyagwa na kupasuka kichwa.
Haikuwa rahisi kuhisi machungu ya watoto hao ambao ni kilio cha muda
mrefu kutoka kwa wazazi na wananchi waishio maeneo ya barabara kuu ya
kuelekea Sumbawanga ambapo takribani watu 18 wakiwemo watoto 10 na watu
wazima 8 hali ambayo imekuwa ikijenga hofu miongoni mwa wakazi wa maeneo
hayo.
Wanafunzi hao walifunga barabara na kulala barabarani kuanzia saa 12:30
alfajiri huku wakihanikiza sauti zao hewani kwa maneno yaliyosikika,
"Tunataka!!, Matuta!!. Magari!!, Yanatumaliza!!!" sauti hizo
zilikaririwa mara kwa mara huku baadhi yao wakionesha mabango.
0 comments:
Post a Comment