Polisi nchini Marekani wamesema kuwa watu tisa wameuawa katika shambulio lililotekelezwa na watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki katika mgahawa wa Twin Peaks uliopo katika jimbo la Texa mjini Waco.
Hata hivyo watu wengine 18 walijeruhiwa vibaya na kupelekwa hospitali kupatiwa matibabu kutokana shambulio hilo.Maofisa wa serikali katika mji huo wanasema kuwa, walibaini mkusanyiko kati ya watu watano walioonekana kupanga jambo lisilo la kawaida.
Watu waliokuwa katika mgahawa huo walijificha katika chumba cha majokofu katika harakati za kujiokoa kabla ya kusaidiwa na Polisi kutoka katika eneo hilo.
PICHA NA DAILY MAIL NEWS
0 comments:
Post a Comment