,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, February 18, 2015




RCP
Na Andrew Chale wa modewjiblog
 
Ile party ya kijanja inayosubiriwa kwa hamu kubwa na watu mbalimbali wa  ndani na nje ya Zanzibar  Maarufu kama ‘RED CUP Party’  kufanyika Februari 28 ndani ya Hoteli ya Palm Beach iliyopo Bwejuu, Unguja.
Akielezea mwandaaji wa shoo hiyo ya kijanja, Djzoro ON Mix Man amesema tayari mipango yote imekamilika na tiketi zimeanza kuuzwa kwa sasa.
“Party ya kijanja ya RED CUP Party,  kwa sasa ni gumzo na tiketi zimeshaanza kuuzwa. Kwa kiingilio cha sh 10,000/= kwa wanaume na  sh  5000/=, kwa wanawake. Pia kwa wanaotaka tiketi wanaweza kuwasiliana kupitia simu namba 0658775755.” Alibainisha Djzoro ON Mix Man
10982328_795315397225783_1381477172125504952_o
Djzoro ON Mix Man aliongeza kuwa,  Party hiyo inayotarajiwa kufanyika katika hoteli ya Palm Beach iliyopo Bwejuu nje ya mji wa Unguja.  Wameandaa magari  yatakayoondokea Ngome Kongwe majira ya  saa 6.  Ambapo pia, kama utakuja na usafiri wako mlangoni  kwenye shoo, kiingilio kitakuwa sh  elf 5 tu sambamba na michezo mbali mbali pamoja na swimming pool.
“Hii shoo ni ya aina yake  kwani ni Kimataifa, tayari set up ya swimming pool ipo tayari kwajili ya REDCUP na usiku zitawaka taa mbali mbali za kupendeza.
Jipange kwa kingilio cha elf 5 mlangon au kwa bus kubwa kutoka NGOME KONGWE mpaka PALM BEACH na shiling elf 10 kwa wanaume na elf 5 kwa wanawake karibu sana” alisema. Djzoro ON Mix Man.
Eneo litakalofanyika Red Cup Party
Eneo litakalofanyika Red Cup Party.
tiketi zipo tayari
Tiketi zipo tayari.

Categories:

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi