
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa
Mh.Mwinyijuma Hamad Mshauri wa kikundi cha Ushirika Cha ufugaji wa
Samaki na Uhifadhi wa Mazingira Gando Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba
akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani
ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010
, Kinana akihutubiwa wananchi leo
katika Wete mjini amewaambia wananchi kwamba viongozi wa Chama cha CUF
wakiwaambia jambo wanatakiwa kuchanganya na akili zao pia ili kutafakari
watakayoambiwa badala ya kukubali kila kitu. Ameongeza kwamba Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mh. Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na
viongozi wenzake wa CUF wapo katika serikali ya umoja wa kitaifa ya SMZ
lakini pamoja na hayo wameshindwa kupekeka Maji, Umeme, Barabara, Afya
na mambo mengine mengi huko Pemba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mabwawa ya kufugia samaki ya kikundi cha kikundi cha Ushirika Cha ufugaji wa Samaki na Uhifadhi wa Mazingira Gando Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa
Mh.Mwinyijuma Hamad Mshauri wa kikundi cha Ushirika Cha ufugaji wa
Samaki na Uhifadhi wa Mazingira Gando Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba na kujionea miti iliyooteshwa katika bustani ya kikundi hicho.
Vijana wakitengeneza maseredani majiko ya udongo katika kijiji cha Chanjaani shehia ya Ukunjwi katika jimbo la Gando.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi majiko
yaliyotengenezwa tayari katika kijiji cha Chanjaani Shehia ya Ukunjwi
Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi aliofuatana nao
wakiangalia mafundi wa Tanesco wakati wakiunganisha umeme katika mradi
wa usambazajiwa umeme jimbo la Mtambwe wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini
Pemba
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiunganisha umeme wakati
aliposhiriki shughuli ya usambazajiwa umeme jimbo la Mtambwe wilaya ya
Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba
Afisa
Uhusiano wa Shirika la Umeme Zanzibar Fakhi Othman Sharif akitoa
taarifa kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati
alipotembelea na kukagua mradi wa Usambazaji wa umeme jimbo la Mtambwe.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki shughuli ya
kuunganisha mabomba ya maji katika mradi wa usambazaji maji jimbo la
Mtambwe Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati, Balozi Amani Karume
kushoto na Mama Maua Daftari kulia wakishiriki kufukia mambomba ya maji
katika mradi huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza taarifa ya Hamiar Adi Makamu Mwenyekiti kuhusu ujenzi wa Maskani ya Jakaya Kikwete Sheia ya Chekea Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo Kinana ameichangia maskani hiyo mabati 50 na mifuko 20 ya saruji.
Mjumbe
wa Kamati kuu ya CCM Ndugu Maua Daftari akizungumza wakati msafara wa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ulipotembelea katika tawi la
Kigangani jimbo la Ole.
Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Ndugu Maua Daftari akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Wete Pemba.
Mkutano huo ukiendelea.
Mohamed Abood Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mtemani mjini Wete Kaskazini Pemba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapa somo wananchi hao waliohudhuria kwenye mkutano huo.
0 comments:
Post a Comment