Gari la mheshimiwa Kassim Majaliwa likiwa eneo la tukio.
Kaa chonjo! Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), mheshimiwa Kassim Majaliwa amejikuta akitumbukia kwenye kamera za Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers baada ya kuchunguzwa kwa kuingia hotelini akiwa ametanguliwa na mrembo mmoja aliyedaiwa kuwa na ahadi naye, Ijumaa Wikienda lina picha kamili.OFM ilimshughulikia waziri huyo juzikati kwenye hoteli ya kisasa ya nyota tatu iliyopo maeneo ya Bamaga-Mwenge jijini Dar es Salaam ambapo mheshimiwa huyo aliingia.
HABARI KAMILI
Majira ya saa 11:05 jioni OFM ilipata taarifa kutoka kwa chanzo chetu kilichopiga simu na kueleza kuwa Waziri Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa, Dodoma ameingia hotelini hapo akiwa ametanguliwa na mrembo huyo.
“Mimi ni msomaji wenu. Niko hapa hoteli ya....(anaitaja jina). Yule waziri wa JK, anayeitwa Kassim Majaliwa amekuja na gari aina ya Toyota Harrier nyeupe, ameshuka na kuingia hotelini. Lakini dakika kumi kabla kuna mrembo mkali ameingia hapa huku anazungumza na simu, nahisi wana ahadi naye,” kilisema chanzo chetu.
SAA 11:10, OFM YATUA HOTELINI
Kikosi kazi cha OFM kilijikusanya na kuingia ndani ya gari kisha yakakanyagwa mafuta hadi kwenye hoteli hiyo ambapo kilishuhudia gari la mheshimiwa huyo likiwa limeegeshwa.
OFM SAMBAMBA NA GARI
Ili kumtega vyema, OFM waliegesha gari lao kwa kupeana mgongo na la waziri na kusubiri kwa muda huku macho ya kamera yakiangalia kwenye mlango mkubwa wa kuingilia hotelini hapo na wakati mwingine kwenye gari la mheshimiwa.
SAA 11: 22, OFM NDANI YA HOTELI
Baada ya kuona muda unakwenda, mmoja wa watenda kazi wa OFM alitoka kwenye gari na kuzama ndani ambapo alipanda mpaka ghorofani kwa lengo la kuchunguza chochote.
OFM ilibahatika kukutana na mhudumu mmoja ambaye alisema hajamuona mheshimiwa huyo, akamshauri kwenda kujaribu kumuangalia upande wa baa, jambo ambalo kachero huyo wa OFM alilifanya.
Mheshimiwa Kassim Majaliwa akipanda kwenye gari hilo.
SAA 11: 26, OFM, WAZIRI MACHO KWA MACHO
Kachero wa OFM alitembea hadi kwenye baa ya hoteli hiyo na kukutana na mheshimiwa ana kwa ana (lakini hawafahamiani).Waziri huyo alikuwa amekaa na wanaume wengine wanne wakizungumza. Mazungumzo yao yaliashiria yana msisitizo kama si umuhimu kwa wote.
0 comments:
Post a Comment