Na Mwandishi wetu
POLISI nchini Ujerumani wamefanikiwa kumkamata Promota mwenye asili ya nchi ya Nigeria ambaye ndiye aliyesababisha fujo katika onyesho la msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ zilizotokea Agosti 30 mwaka huu kwenye ukumbi wa Stuttgart nchini Ujerumani .
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka nchini Ujerumani kilisema kwamba Jeshi la Polisi nchini humo kilisema hadi kieleweke kwani watamchukulia hatua kali ili iwe fundisho kwa mapromota kama huyo.
Jumamosi iliyopita Awin Williams Akpomie (pichani) alisababisha fujo na kuvunjwa kwa viti , vyombo vya muziki na vitu mbalimbali baada ya mashabiki kushikwa na hasira kwa kukosa burudani ya shoo ya Diamond ambapo alicheleweshwa na Promota huyo aliyewatangazia shoo kuanza kufanyika saa nne usiku na badala yake kutaka shoo ifanyike saa kumi alfajiri.
Baada ya uchunguzi wa polisi kufuatia fujo hizo imegundulika kuwa muandaaji wa onyesho hilo Akpomie aliudanganya utawala wa ukumbi wa Sindfingen kwa kukodisha ukumbi huo kwa ajili ya African Party na mkutano sio onyesho la muziki kama alivyofanya,na kusababisha fujo zilizotia hasara kiasi cha Euro 300,000 sawa na sh. Mil.600 za Kitanzania ambazo anatakiwa azilipe.
Aidha imeelezwa kwamba Akpomie hakuwa na bima ya kulinda onyesho hilo na ukumbi lilipotarajiwa kufanyika onyesho hilo ambapo ni ukumbi wa mikutano na maonyesho ya bidhaa siyo muziki.
Taarifa za kipolisi zinasema kwamba suala hilo tayari zimepeleka suala hilo kwa ofisi ya Sheria ya mji wa Stuttgart zilikotokea fujo hizo ili sheria ichukue mkondo wake.Hadi sasa bado Polisi wanaendelea kumhoji Akpomie kutokana na tetesi kwamba najihusisha na biashara zingine za haramu.
Wakati huo huo Taasisi mbali mbali na jumuiya za Wafrika nchini Ujerumani na jirani zimelaani vikali tabia za raia huyo wa Nigeria Akpomiemie kwa kuwadanganya mashabiki na kulivunjia hadhi sifa za bara la Afrika nchini humo , pia taasisi na jumuiya hizo zimewaonya watu kujiepusha kabisa .
0 comments:
Post a Comment