,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, September 9, 2014

Felista_street talk ELIMU ya Asayansiinayotolewa  kwa wanafunzi  wa shule za
  sekondari mkoani Arusha
  kupitia sanaa ya maigizo inayoelezea chimbuko la binadamu 
  imekuwa ikisaidia 
  kuongeza uelewa na mwamko wa wanafunzi kupenda masomo ya
  sayansi.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa Idara ya makumbusho ya
  elimu viumbe ,mkoa wa Arusha, Felista
  Mangalu, kwenye maonyesho ya sanaa ya sayansi ya chimbuko la
  binadamu kwa shule
  za sekondari yanayotolewa na kikundi cha sanaa cha
  Scatterlkingis  cha
  Afrika kusini.

Mangalu,alisema kuwa ufundishaji wa sayansi kupitia
  maonyesho ya sanaa ni mbinu mpya inayosaidia
  wanafunzi kuyapenda zaidi masomo ya sayansi, na kutambua
  kuwa sayansi ni ajira.
Alisema kuwa kikundi hicho kimeshatoa  elimu hiyo kwa shule
  kadhaa za sekopndari za
  jijini Dar es Salaam, Karatu na Ngorongoro,ambapo wanafunzi
  wamekuwa na mwamko
  mkubwa wa kupenda masomo ya sayansi.
Amepongeza kuwa hii ni mara ya tatu kwa kikundi hicho cha
  sanaa kutoka nchini afrika kusini
  kufanya kufundisha sayansi kwa kutumia sanaa ya maigizo 
  ,ambapo wanafunzi
  wa sekondari kutoka shule mbalimbali za Arusha huwa
  zinakusanyika makumbusho na kupata elimu hiyo.
Awali kiongozi wa kikundi hicho ,cha sanaa   cha
  Scatterlings,Profesa Robart Blumen Schine ,amesema kuwa
  kupita  sanaa wanafunzi wanaelewa chimbuko la binadamu na
  mabadiliko yaliyotokea hadi kufikia kwenye sayansi na
  teknolojia.
Alisema kuwa  Tanzania inao utajiri  mkubwa wa mambo ya
  kale hasa
  katika maeneo ya 0lduvai Georg na Laitory,na wanaendeleza
  juhudi za kuelimisha
  wanafunzi kupitia sanaa ili waweze kuelewa historia nzima ya
  chimbuko la
  binadamu kutoka hatua za mwanzo hadi kufikia ustaarabu.
Profesa,amesema kuwa kutumia sanaa wanfunzi wamekuwa na
  mwamko mkubwa wa kupenda
  sayansi na hivyo wanakuwa na uelewa wa hali ya juu wa
  chimbuko la binadamu
Kwa upande wake Afisaa wa mpango wa elimu ya viumbe wa
  makumbusho hiyo,Bura
  Akonay,  alisema kuwa binadamu tumebadilika kutoka hatua 
  mbalimbali
  za mabadiliko ambayo yamewezesha binadamu kukabiliana na
  mabadiliko hayo.
Amesema makumbushohiyo ni kitivo cha  chimbuko la
  mabadiliko  ya binadamu kutoka enzi
  ya zana butu za mawe hadi kufikia kutengeneza vifaa bora vya
  kisasa kwa kutumia teknolojia.
Akonay,amesema njia hii ya kufundisha sayansi kwa kjutumia
  sanaa  inarahisisha na kuthibitisha
  uwepo wa  mabadiliko ya binadamu  kutoka hatua moja kwenda
  nyingine .
Ameongeza kuwa binadamu tumetoka asili moja  na tumekuwa
  tukibadilika kutoka hatua moja
  hadi nyingine na hali hiyo inasababisha tuweze kuyakabili
  mazingira yetu .
Ameongeza kuwa kusoma kwa kupitia sanaa kutasaidia kuwavutia
  zaidi wananzi kusoma sayansi na kuwa
  na kumbu kumbu nzuri ya chimbuko la binadamu.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi