Marin Cilic aibuka bingwa
Marin Cilic wa Croatia ameibuka bingwa wa US Open kwa kumfunga Kei Nishikori wa Japan
Mpambano huo umechezwa katika uwanja wa Arthur Ashe Mjini New York Marekani.
Cilic
amepokea kombe la michuano ya tennis upande wa wanaume kwa mara ya
kwanza baada ya kumshindilia mpinzani wake seti tatu za 6-3, 6-3 , 6-3.
Hii
ni mara ya kwanza katika historia ya fainali za US Open ambapo mchezo
wa mwisho unawakosa mmoja kati ya wachezaji wakali akiwemo Andy Murray,
Novak Djokovic ama Roger Federer.
Cilic anakuwa Mkroatia wa kwanza
kutwa ubingwa wa moja kati ya mashindano makubwa manne ya tenis duniani
tangu kocha wake Goran Ivanisevic abebe ubingwa wa Wimbledon mwaka 2001
0 comments:
Post a Comment