People's Power ni Ideology made kwa
ajili ya Mataifa ambayo hayana Demokrasia, kama vile The Arab World,
lakini sio kwa Taifa kama letu la Tanzania. Hapa we are enjoying a full
Democracy, kwa hiyo ni muhimu sana kwa Chama changu CCM, kusimama kidete
na kuikataa sera ya People's Power iliyoletwa na kuongozwa na Chadema,
baada ya sera zao za Majimbo na Mafisadi kushindwa kutoa results.
Tanzania tunaongozwa na sera ya Mihimili mitatu, nayo ni Ikulu,
Mahakama, na Dola as opposed na maneno ya wengi kwamba tunaongozwa na
Ikulu, Bunge na Mahakama. Pia kwenye the end kuna sisi wananchi. Sasa
CCM tunahitaji kua makini sana kwa sababu, ili People's Power ifanikiwe
ni lazima Rais wa sasa apunguziwe Madaraka, kitu ambacho Chadema
wamekuwa wakikililia sana kwenye mikutano ya Katiba mpya, ni kwa sababu
wanajua kwamba Rais akipunguziwa madaraka wataweza kujipenyeza na
kugonganisha mihimili hii ya Serikali na kuweza kushika nchi kirahisi
sana kwa njia kama zile zilizotumika Egypt na Tunisia.
CCM we don't seem to understand the game
Chadema is playing nyuma ya pazia la People's Power na hatari zake kwa
Taifa na hasa maendeleo ya CCM kama chama Tawala. Kazi muhimu ya chama
chochote Duniani ni kushinda uchaguzi kwanza, and then kutawala. CCM we
need to educate our members athari za Rais wetu kupunguziwa madaraka,
sawa kuna areas ambazo ni kweli anahitaji kupunguziwa, lakini bado ni
lazima tupigane mpaka mwisho wa vita hivi vya itikadi, kuhakikisha
mabadiliko ya katiba hayaondoi madaraka ya Rais kuchagua Viongozi wa
Jeshi, Polisi, Mahakama, na pia tusijidanganye hata siku moja kufikiria
kuwa na Rais wa CCM, asiyekuwa Mwenyekiti wa CCM siku tutakapojidanya na
hilo ndio utakuwa mwisho wetu wa kutawala taifa hili.
Nia na madhumuni ya People's Power, ni
kuwahamasisha wananchi wa-raise against Serikali, kama ilivyofanyika
Egypt na Tunisia, na hii ni baada ya Chadema kugundua kwamba hawana
uwezo wa kuishinda CCM kwenye kura. Kwenye uchaguzi uliopita Chadema
walidai walishinda Urais, which was a pure nonsense, kwa sababu huwezi
kushinda Urais wa Tanzania huku ukiwa na Wabunge 46 tu kati ya Wabunge
357 wanaotakiwa kisheria ya Jamhuri. Kwa hali ya kawaida haiwezekani
wananchi wakapigia kura wabunge wengi wa CCM, lakini wakapigia kuchagua
Rais wa kutoka Chadema kwenye kura hiyo hiyo. Sijawahi kumsikia Dr. Slaa
mwenyewe akisema aliibiwa Urais kwa kawaida hayo husemwa na wapambe
wake lakini sio yeye mwenyewe ikiwa ni dalili tosha kwamba anajua ukweli
kwamba hakushinda. Lakini kulalamika kila wakati ni moja ya mbinu za
kisiasa za Chadema kutaka kukubalika kwa wananchi.
Ninasema CCM, we cannot afford kulala na
hawa Chadema, they are serious na wako very hungry na madaraka ambayo
wanajua kabisa kwamba hawayawezi, kwa sababu hata kukiongoza chama chao
wameshindwa, ndio maana leo unaona kina Zitto na Shibuda wanatangaza
mapema kutaka kugombea Urais kupitia huko bila kusubiri vikao vyao, ni
kwa sababu wanajaribu kutumia nguvu ya umma yaani wananchi kuwashinikiza
Chadema watumie Demokrasia wakati utakapofika wa kuchagua mgombea wao.
CCM tukiruhusu kushindwa na Chadema 2015 tutakuwa tumewasaliti wananchi
wa Tanzania, ambao wengi wao hawajui nia na madhumuni ya Chadema, ambayo
ni simply Madaraka na Biashara tu kwa watu wachache ndani ya uongozi wa
juu wa chama chao.
Ni matumaini yangu kwamba CCM,
tutajipima na kujitafakari sana namna ya kwenda mbele na sera za
Chadema, ambazo ni hatari sana kwa taifa letu. CCM tuwaelimishe
wanachama wetu waweze kujadili siasa za taifa kwa uelewa zaidi kuliko
ki-Yanga na Simba kama wanavyofanya sasa. Halafu pia CCM ni lazima
tuimarishe dhana za kujipima ndani ya Chama kwa viongozi wasiojiweza
kiuongozi, tumejaza wengi sana ndani ya chama chetu, ninatoa pongezi
sana kwa NEC kwa jinsi ilivyoweza kusimamia zoezi la kupitisha majina
majuzi Dodoma. Wamejitahidi sana kupunguza makenge wengi kwenye huu
msafara wetu wa Mamba, ingawa bado kuna makenge wengi bado wamerudi,
lakini ninaamini kwamba kati ya sasa na 2015, wengi wao watajipima na
kuachia ngazi wenyewe.
MUNGU AIBARIKI TANZANIA!!
William Malecela Le Mutuz!!

Umesema jambo sahihi. Kwa kuisaidia CCM kushinda, inabidi pia serikali yake ijitahidi kufanya kazi za kimaendeleo. Wananchi wakiridhishwa mahitaji yao ( umeme, maji, miundo mbinu bora na elime kwa watoto wao) hakutakuwa na haja ya kampoeni kali kwa kugombea urais. Tafadhalini tekelezeni hayo.
ReplyDeleteChadema wanasikitisha sana wanavyoendekeza wananchi kuvunja baadhi ya sheria za nchi, kwa mfano hili lililotokea jana Iringa. Manispaa imeweka mahali pa kufanyia biashara ndogo ndogo, sasa kwa nini tena mbunge anawaambia wavunje sheria na kuanika biashara zao popote? Chadema wanajua kuwa vijana wakivunja sheria polisi watatokeza sasa nia yao ni nini kama siyo kuvuruga amani?