TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Chama
Cha Mapinduzi kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kuvamiwa, kupigwa
na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) na Mhariri
Mtendaji wa New Habari 2006 Ndugu Absalom Kibanda usiku wa kuamkia
Jumatano Machi 6, 2013.
Chama Cha Mapinduzi kinalaani kwa
nguvu zote kilichotokea kwa Absalom Kibanda, kwani ni unyama
usiokubalika hata kidogo, unafaa kulaaniwa na Watanzania wote.
CCM tunaitaka Serikali kuhakikisha
inawapata waliofanya unyama huo na kuwafikisha mbele ya vyombo vya
sheria ili sheria ifuate mkondo wake, na kukomesha matukio ya namna
hiyo.
Aidha, Chama Cha Mapinduzi kinatoa
pole kwa Uongozi wa Jukwaa la Wahariri, Afisa Mtendaji Mkuu wa New
Habari 2006, familia ya Ndugu Kibanda, wanahabari na wadau wote wa
habari nchini, na tunamwombea kwa Mwenyezi Mungu apone haraka na kurejea
katika kazi zake za Ujenzi wa Taifa.
Imetolewa na:
Nape M. Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UEENEZI
08/03/2013
0 comments:
Post a Comment