- Najua kwamba siasa ni mchezo mchafu ila sometimes watu ndio huwa wanakuwa wachafu na tunaisingizia siasa.
Nimeshtushwa sana na simu za marafiki zangu mbalimbali wakiniuliza kama ni mimi kweli ndie ambaye nimeandika na kupost kule Jamiiforum WARAKA KWA KATIBU MKUU WA CCM TAIFA juu ya malalamiko na tuhuma mbalimbali dhidi ya vikao vya chama na viongozi wake juu ya nafasi ya Mwenyekiti UVCCM kwenda Zanzibar katika uchaguzi unaokuja.
Bahati mbaya sana sikupata bahati kuisoma habari hiyo zaidi ya kuambiwa na watu,kwasababu nilikuwa safarini na kwa bahati mbaya kabisa sikuwa na nafasi ya ku-access jamiiforum lakini baada ya kufika salama nikaingia jamiiforum nikakuta tayari imeshafutwa.
Niwaombe radhi rafiki zangu wote na vijana wenzangu wa uvccm, kwa usumbufu mlioupata kutokana na habari hiyo na ukimya wangu ambao uliwafanya msijue ukweli ni upi.
Sijawahi kulalamika wala kuandika waraka kwa viongozi wangu wa chama kama ilivyoonekana leo jamiiforum kupitia account fake ya mtu anaitwa Ndg Al Saad ambaye anataka kuwaaminisha watu kwamba huyo ndo Anthony Mavunde,nikiwa kama kiongozi nafahamu utaratibu wa kichama wa kuwasilisha malalamiko(ambayo sina),chama hakijawahi kuendeshwa kupitia social media,wanaofanya hivi ni kikundi cha watu wenye nia ya kunichonganisha mimi na viongozi wangu wa Chama pamoja na vijana wenzangu wa Zanzibar lakini mbaya zaidi ni kunihusisha na hoja ya UAMSHO ya Zanzibar.Huu ni umaskini mkubwa sana wa mawazo na ishara ya wazi kwamba mwandishi anatumika kwa maslahi binafsi.
Mwisho,kabisa niwaombe tu hicho kikundi ambacho kinatumiwa kwa maslahi binafsi ya watu pamoja na huyo kiongozi wenu ambaye anawapa maelekezo,mtafakari kwa kina harakati zenu chafu ambazo mnafanya juu yangu maana heshima yenu mbele ya jamii inazidi kushuka.Najua hapa tatizo ni uchaguzi wa Vijana unaokuja ndio unasababisha haya yote.
Naomba Mwenyezi Mungu aendelee kunipa moyo wa uvumilivu na kukabiliana na changamoto nyingi zinazokuja.
Vox populi Vox Dei "sauti ya wengi,ni sauti ya Mungu"

0 comments:
Post a Comment