Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Farreo (kushoto) akimshuhudia Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huawei Mengdong Gao,(kulia) akimkabidhi jezi nahodha wa timu ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc, Ngayama Matongo (katikati) wakati wa mchezo wa kirafiki baina ya kampuni hizo,uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, Vodacom Tanzania Plc ilishinda magoli 7-1.
Kikosi cha timu ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC, wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Ian Ferrao(katikati) aliyeshika mpira wakipozi kwenye picha kabla ya kuanza kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya kampuni ya Huawei uliofanyika kwenye viwanjwa vya Gymkhana jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Vodacom Tanzania iliilaza Huawei magoli 7-1.
Wachezaji wa timu ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC, wakishangilia ushindi wao baada ya kuiadhibu timu ya wafanyakazi wa Huawei mabao 7-1 wakati wa mchezo wa kirafiki ulifanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment