

Remidius Mwema Emmanuel
# SHUKRANI MHE. ANTONY MAVUNDE#
"Ikiwa ni sehemu ya majukumu yangu ya Kikazi kama Katibu Mkuu wa Shirikisho la Jumuiya za Wanafunzi watanzania wanaosoma Jamhuri ya watu wa China (TASAFIC), Leo 28 Agosti, 2017 nimemtembelea na kufanya mazungumzo na Naibu waziri wa Vijana,Ajira na Kazi Mhe. Anthony Mavunde ."
Pamoja na mambo mengine Mhe. Mavunde amepokea Maelezo mafupi juu ya Mkakati wa Shirikisho (TASAFIC) kwa Vijana wa Kitanzania wanaohitimu masomo yao nchini Chini wanavyoweza kuwa chachu ya Mabadiliko ya fursa mbalimbali hapa nchini kutumia Uzoefu na taaluma wanayoipata baada ya kuhitimu Elimu yao.
Kwa upande wake Mhe. Mavunde amepongeza juhudi zinazofanywa na TASAFIC na kuongeza kuwa Serikali iko tayari na inaendelea kuwaunga mkono Vijana wote wanaoonyesha uthubutu wa kujikwamua kiuchumi. Akizungumzia Upande wa kilimo, Amesema baadhi ya Vijana wamekuwa na mitizamo ya kutojihusisha na Kilimo, Lakini hii inatokana na wengi wao kujaribu kilimo kwa kutozingatia kanuni na Misingi bora ya Kilimo na kuona jambo hilo haliwezekani,.
"Serikali sasa tuna mikakati ambayo tuna hakika itasaidia kuondoa dhana hizo na kuwafanya vijana wengi kupenda kilimo ikiwa ni pamoja na Kutoa Elimu zaidi na kuwatumia vijana waliofanikiwa kuweza kuaelimisha wenzao...Mfano tunao vijana wahitimu wa Chuo kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) wanaitwa SUGECO, Serikali iliwapatia udhamini wa fedha kupitia Benki ya CRDB, wakafanya kilimo na sasa wamekuwa ni taasisi kubwa na wameanza kusaidia vijana wenzao kupitia mafunzo na misaada mbalimbali. Lakini wapo vijana Mkoani Mbeya, Ruvuma na mikoa mingine ambao wamepata mafanikio makubwa. Jambo la msingi ni vijana kubadili mitizamo, tunayo Benki yetu ya maendeleo ya kilimo, Mifuko ya pembejeo, Mifuko ya uwezeshwaji wananchi na mfuko wa maendeleo ya Vijana hiyo ni hatua mojawapo lakini bado Serikali inafanya juhudi kubwa kuhakikisha vijana kupitia vikundi rasmi wanajenga utayari wa kujihusisha na kilimo, hata kilimo cha muda mfupi (Mboga mboga) ambacho pia kimeleta manufaa makubwa kwa makundi ya Vijana" Alisema Mhe .Mavunde
Nami nimemhaidi Mhe .Naibu waziri kuhakikisha Naendelea kuwajibika kuwatumikia watanzania Wote wanaosoma Jamhuri ya watu wa China (Kupitia wadhifa wangu) Kwa kushirikiana na Viongozi wenzangu na pindi nitakaporejea China nitafikisha ujumbe wake Kwa wasomi hao,Ikiwa ni pamoja na kuielezea vyema na kuwakumbusha fursa njema na mikakati ya Serikali yetu iliyopo pindi watakapohitimu Masomo yao na kurejea nchini (Tanzania).
0 comments:
Post a Comment