Mwigizaji wa kitambo wa tamthiliya na sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
UBUYU
wa Zanzibar upo wa aina nyingi. Kuna uliotiwa hiliki, mwingine
unachanganywa na mdalasini. Lakini ubuyu wa leo ni ule uliotiwa pilipili
mtama na tangawizi. Ukiumung’unya sharti mdomo ukucheze! Upo hapo?
Ubuyu huu si mwingine bali ni wa mwigizaji wa kitambo wa tamthiliya na
sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
MAHABA SIYO YA NCHI HII
Ubuyu
ulionyakwa na safu hii unadai kuwa, Johari kwa sasa amenasa kwenye
penzi jipya na jamaa ambaye jina halikupatikana mara moja hivyo
linafanyiwa kazi, lakini ishu ni kwamba wanadaiwa kuwa kwenye mahaba
mazito ambayo siyo ya nchi hii. Chanzo makini kilichomwaga ubuyu huu
kwenye ungo kwa ajili ya watu kujinafasi kilitonya kuwa, Johari na
mwanaume huyo anayesemekana ni bonge la mtanashati, huwa mara nyingi
wanapenda kujivinjari kwenye ‘pub’ mpya ya mwigizaji matata wa Bongo
Movies, Irene Uwoya iitwayo Left Minutes iliyopo maeneo ya Sinza-Mori
jijini Dar
Blandina Chagula ‘Johari’ akiwa na anayedaiwa kuwa mpenzi wake.
JOHARI AMEPATA POZO LA MOYO?
“Unaambiwa
bidada Johari sasa hivi amepata pozo la moyo wake. Yaani huyo kaka
anampenda Johari hadi raha na hapa nafikiria kabisa wana mpango wa
kufunga ndoa. “Ukitaka kujionea mambo mara nyingi utawakuta pale kwenye
baa ya Uwoya na muda wote wanapokuwa pamoja wanakuwa kwenye mahabati
mazito,” kilinyetisha chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa gazetini.
Mnyetishaji
huyo alidondosha ubuyu kuwa, mtu ambaye huwa anapenda kuwaweka kwenye
ukurasa wake wa Snap Chat ni Uwoya ambaye anaonekana kuubariki uhusiano
huo. Ijumaa Wikienda, kama kawaida yake, baada ya kupata ubuyu huo mtamu
lilifunga safari hadi kwenye baa ya Uwoya na kuzungumza na
‘mashushushu’ wake ambao walikiri kumuona staa huyo na ‘bebi’ wake huyo
mpya (new brand).
Baada
ya Ijumaa Wikienda lilimtafuta Uwoya ambaye anatajwa kuwa ‘kiunganishi’
na msiri mkubwa wa Johari na pia anawaposti kwenye mtandao ili aweze
kufafanua juu ya kinachoendelea. Katika majibu yake, Uwoya hakukataa
wala kukiri kuwepo kwa uhusiano huo, lakini alisema yeye hawezi kujua
hata siku moja kitu ambacho kipo mioyoni mwa watu. “Jamani kwani mimi
siruhusiwi kumposti mtu picha yake akiwa hata na jamaa yake? Maana hao
kama wana uhusiano wa kimapenzi mimi sina uhakika na hilo,” alisema
Uwoya.
Ijumaa
Wikienda halikuishia hapo, bali lilifunga safari kumsaka Johari ili
kumfungukia mwanaume huyo ambapo mambo yalikuwa hivi; Ijumaa
Wikienda: Mambo Johari, vipi kuhusu mipango ya ndoa na shemeji yetu mpya?
Johari: Shemeji? Yupi huyo tena?
Ijumaa Wikienda: Kwani wapo wangapi wapya? Namaanisha huyo unayejiachia naye kwenye baa ya Uwoya na kujiachia.
Johari: Jamani…mhhh…hapana… huyo siyo mtu wangu mimi. Ijumaa Wikienda: Mbona mnaonekana mkiwa kwenye mahaba mazito?
Johari:
Duh! Hebu naomba nipigie baadaye kidogo tutazungumza. Hata hivyo, baada
ya saa kadhaa, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Johari kwa mara nyingine
ambapo hakupokea simu na hata alipotumiwa chatting kwenye WhatsApp
hakujibu.
KUTOKA DAWATI LA UBUYU
Ijumaa
Wikienda ni kijumbe tu katika kuufikisha ubuyu kwa wamung’unyaji hivyo
kilichobaki ni macho ya watazamaji na masikio ya wasikilizaji kuona
kitakachojiri kwani kwa muda mrefu Johari amekuwa akisaka wa kupooza
mtima wake.


0 comments:
Post a Comment