MAMLAKA ya Maji safi na Maji taka Jijini Dar es Salaam (DAWASA) imetoa taarifa kwa uma kuwa imekamilisha miradi ya maji na kuongeza hali ya upatikaji wa maji katika jiji la Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Kaimu Katibu Mkuu wa Dawasa Romanus Mwang'ingo amesema wamekamilisha mradi huo kutoka uzalishaji wa maji mita za ujazo 180,000 hadi 270,000 pamoja na ulazaji wa bomba kuu la mita 1.8 kutoka Ruvu chini hadi matenki ya Chuo kikuu cha Ardhi.
Hata hivyo amesema mradi huo ni pamoja na Ofisi za kuendeshea mradi, ujenzi wa tenki la kuhifadhia maji la ujazo wa mita milionii 10 la Kibamba ikiwa pamoja na Ofisi ya uendeshaji huduma za maji Kibaha.
'Tumekamilisha na ujenzi wa nyumba za wafanyakazi katika mtambo wa Ruvu juu na hata ule wa njia mpya ya umeme wa msongo mkubwakutoka Chalinze hadi Mlandizi" alisema.
Amesema lengo la mradi huo ni pamoja na kuhakikisha kuwa wananchi wa kawaida, wenye viwanda na biashara katika eneo la mradi watapata huduma bora za maji haswa baada ya maji kuongezeka.

0 comments:
Post a Comment