Mahakama ya hakimu mkazi kisutu leo imepokea taarifa ya Mkemia Mkuu wa Serikali ikionyesha sampuli ya mkojo wa Video Queen asiyeishiwa na vituko Agness Masogange. Taarifa hiyo iliyo wakilishwa na Wakili wa Serikali Constantine Kakula mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri.
Ushahidi huo umetolewa na shahidi namba moja kwenye kesi hiyo Elia Mulima ya kwamba mshatkiwa alipewa kontena kwa ajili ya kuwekea sampluli ya mkojo, huku akisimamiwa na Askari Polisi wa kike.
Hata hivyo mahakama imepokea sampuli hiyo kama kielelezo namba moja cha ushahidi na kutupilia mbali pingamizi la upande wa utetezi kuwa fomu zilizopelekwa kwa mkemia mkuu hazikufata sheria.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 31, mwaka huu.

0 comments:
Post a Comment