Elizabeth
Michael (Lulu) amedai ndoa yake na mpenzi wake Dj Majay
inakaribia.Muigizaji huyo ambaye ameonekana kutulia sana tangu alipokuwa
na mahusiano na bosi huyo wa EFM na TVE amesema hivi karibuni wale
waliokuwa wakitaka waachane watabaki midomo wazi.
“Siku
zinakaribia na karibu tarehe ya ndoa yangu itatangazwa kwa uwezo wa
Mungu. Hapo ndipo waliotamani tuachane wataziba midomo, maana natarajiwa
kuwa mke halali hivi karibuni,” ameliambia gazeti la Mtanzania.
Lulu ameongeza kuwa anatamani kuwa mke bora kwenye ndoa yake kama alivyokuwa sasa kwenye mahusiano yake.
0 comments:
Post a Comment