Castle Lite wametangaza kumshusha Bongo mmoja kati ya A List Artists kutoka maandishi matatu U.S.A, Future ambaye kwa sasa ana hit na ngoma yake ya Mask Off.Ni katika show ambayo inatarajiwa kufanyika tarehe 22 ya mwezi July mwaka huu pande za Leaders Club Dar es Salaam ambapo Future ataungana na msanii Diamond Platnumz kutoka hapa hapa Tanzania katika kudondosha mvua ya Burudani siku hiyo.
Pia Diamond Platnumz amelithibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa instagram kwa kuandika kwamba “DAR ES SALAAM!!!!! DAR ES SALAAM!!!!!! YOU KNOW HOW MUCH, I’VE BEEN MISSING YOU, RIGHT???????? SEE YOU AT LEADERS CLUB ON THE 22ND OF JULLY 2017 THEN!!”
0 comments:
Post a Comment