,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, March 10, 2017

Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye umri wa miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys inataraji kuanza kambi mpya Machi 12, mwaka huu jijini Dar es Salaam kutokana na mabadiliko yaliyofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) .


Serengeti Boys itaanza kwa kuweka kambi jijini Dar es Salaam kwa siku 14 na baadae itakwenda Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya mechi za kirafiki za kimataifa kujiandaa na michuano Afrika ambayo sasa itaanza Mei 14, 2017 badala ya Mei 21, mwaka huu.

 Michezo ya kirafiki ya kimataifa itakuwa ni dhidi ya timu za vijana za Rwanda (Machi 28, 2017), Burundi (Machi 30, mwaka huu) na Uganda Aprili 2, mwaka huu). Michezo yote itafanyika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera. 
Sababu za kuwa na mechi hizo Bukoba ni kupunguza gharama kwa TFF kwani ni rahisi kusafirisha timu hizo kutoka nchi jirani za Rwanda, Burundi na Uganda.

Timu hiyo itarejea tena Dar es Salaam Aprili 3, mwaka huu ambako siku inayofuata itaagwa kwa kupewa bendera na mmoja wa viongozi wa nchi kabla ya kusafiri Aprili 5, mwaka huu kwenda Morocco kwa ajili ya kambi.

Timu hiyo itaunganisha kwenda Cameroon Mei mosi, mwaka huu ambako Mei 3, 2017 itacheza mechi ya kwanza na Cameroon kabla ya kurudiana Mei 6, mwaka huu na siku inayofuata itakwenda Gabon.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi