Takwimu zilizotolewa na WADA zilionesha kwamba
zaidi ywa wanamichezo 1,000 walinufaika kwa namna moja au nyingine kutokana na
matumizi ya dawa zilizokatazwa michezoni kti ya mwaka 2011 - 2015.
Kutokana na tatizo hilo kuonekana kuwa kubwa nchini
Urusi viongozi wa michezo mbalimbali
nchini humo wameahidi kupigana katika vita hiyo dhidi ya dawa zilizopigwa
marufuku michezoni.
Ngili amesema jitihada zinazofanywa na Urusi ni ndogo na haziendani
kabisa na kasi ya upigaji vita wa dawa za kusisimua misuli ndio sababu
wanamichezo mbalimbali wa Urusi wamepigwa marufuku ya kushiriki katika michezo mbalimbali.
Miongoni mwa wanamichezo hao ni pamoja na wanariadha ambao wamepigwa
marufuku na Chama cha Mchezo wa Riadha duniani IAAF
Kuhusu mchakato wa ushiriki wa Urusi kupewa nafasi
ya kushiriki katika michezo ya Olimpiki ya majira ya joto mwakani Katibu huyo
amesema watatazama kama hilo litawezekana, lakini kubwa ni kwamba litategemea
na jitihada watakazozionyesha katika upigaji vita wa dawa za kusisimua misuli.
Wakati huo huo Urusi imeandaa mpango wa kuweka mabango pembezoni mwa
barabara kama sehemu ya kuonyesha hisia zake juu ya upigaji vita dawa hizo.
0 comments:
Post a Comment