,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Thursday, March 9, 2017

MSANII wa muziki Bongo, Sister Fay ambaye siku chache zilizopita aliingia kwenye mgogoro na msanii mwenzake Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kwa madai ya kumtelekeza mtoto aliyezaa naye aitwaye Prince, hatimaye ameafikiana na Fay kuwa atamsomesha.

Baada ya kutokea sekeseke hilo walikubaliana kufanya kipimo cha DNA ambapo mara ya kwanza zoezi hilo halikufanikiwa na kukubaliana kufanya baada ya wiki mbili kwa maana ya wiki hii, ndipo mwanadada huyo akafunguka kuwa hawawezi kupima tena kwani Nay kakubali kumsomesha mtoto.
“Ni kweli tulikuwa kwenye mpango wa DNA lakini Nay kakataa kaona aina haja, kakubali kumsomesha mtoto, namshukuru Mungu kufikia hatua hiyo, naamini kila kitu kitaenda sawa,” alisema Sister Fay.
Kwa upande wa mtuhumiwa, Nay wa Mitego alipotafutwa kwa njia ya simu iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno, hakujibu.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi