Majiji
ya Paris na Los Angeles yameonyesha nia ya kuandaa michuano ya Olympics pamoja
na michuano ya wachezaji wenye ulemavu ya Paralympics ya mwaka 2024 na sio
michuano ya 2028.
Hata hivyo kamati ya kimataifa ya
Olimpiki imeonyesha nia ya kuipa miji hiyo nafasi ya kuandaa michuano ya
olimpiki ya mwaka 2024 na 2028 mwezi September.
Mpiga makasi wa Ufaransa Tony Estanguet amesema wakati sahihi kwa jiji la paris kuandaa
fainali hizo ni mwaka 2024 na kama hilo litashindikana anaona itakuwa sio
rahisi kwa jiji hilo kuandaa tena fainali za michuano ya olimpiki.
Tony Estanguet amesema kuandaa michuano hiyo kwa mwaka 2024
itakuwa ni rahisi kwani miundo mbinu iliyopo inaweza kutumika lakini jiji hilo
halina fungu kwaajili ya kuandaa michuano hiyo mwaka 2028.
Sababu hasa ya jiji la paris
kutaka kuhodhi michuano hiyo kwa mwka a2024 ni kwasababu serikali ya nchi hiyo
ipo tayari kutoa ushirikiano kwa asilimia 95%.
Kwa upande wa kamati ya olimpiki
ya jiji la Las Angels imejipigia chapuo kwa kusema kwamba michuano hiyo
ikifanyika katika jiji hilo itakuwa imefanyika katika jiji sahihi kwa muda
sahihi.
Maandalizi katika jiji hilo yako
tayari kwa asilimia 88% kwani miundombinu itakayotumika ni miundombinu ya uma
huku swala la usalama nalo likichukua nafasi kubwa.
Hata hivyo kumekuwepo na taarifa
zinazosema kwamba jiji litakalokosa nafasi ya kuandaa michuano hiyo mwaka 2024 litapewa
fursa ya kuandaa fainali hizo mwaka 2028.
Kura ya nani atakayepata fursa ya
kuandaa michuano ya mwkaa 2024 inataraji kuamuliwa na wajumbe wa kamati ya
kimataifa ya Olimpiki IOC.




0 comments:
Post a Comment