Leo March 8 Dunia nzima inaadhimisha siku ya Wanawake Duniani, siku ambayo ni special kwa kuangalia na kuyasherehekea makubwa ambayo yamefanywa na Wanawake Duniani kote.Kibongo bongo mrembo Wema Sepetu ameamua kuiadhimisha siku hiyo kiaina yake. Ikiwa ni baada ya kuamua kuungana na wanawake wenzie mkoani Morogoro na kuendesha zoezi la upandaji wa miti katika maeneo tofauti tofauti mkoani humo. Ikiwa lengo kuu la zoezi hilo ni kupambana na tatizo la uhaba wa maji siku za usoni.
Wema Sepetu alitusnua kuhusiana na mchongo huo kupitia page yake ya instagram baada ya kupost baadhi ya picha zinazo muonyesha akiwa katika zoezi hilo.
0 comments:
Post a Comment