,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, March 10, 2017


Klabu ya Azam FC imekamilisha maandalizi yote kuelekea katika mchezo wao wa siku ya Jumapili dhidi ya klabu ya Mbabane Swallows katika mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi.


Akizungumzia maandalizi ya Azam Afisa Habari wa Azam FC Japhary Iddi Maganga amesema tayari maandalizi ya awali yameshakamilika na kikosi cha klabu hiyo kilichopo chini ya kocha Aristica Cioaba kipo katika hari ya juu ya kutafuta matokeo katika mchezo wao wa awali.

Japha amesema mchezo huo utapigwa majira ya saa moja na robo usiku ili kutoa fursa kwa watanzania wengi kujitokeza kushuhudia mchezo huo, huku akiwataka wapenzi na wadau wa soka wakate tiketi mapema kuepuka usumbufu kwani uwanja wa Azam Complex una uwezo wa kuchukua mashabiki 700 tu.


Katika hatua nyingine Japha amewataka watanzania wajitokeze kwa wingi pia katika mchezo unaoikutanisha klabu ya Yanga dhidi ya Zanaco kwani ushindi wa Yanga ni ushindi wa watanzania.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi