Wakazi wa wa miji ya pembe tatu wakijiandaa na theluji iliyoanguka usiku wa kuamkia Jumamosi Jan 7, 2017. miji iliaathirika kwa theluji nyingi ni Burlington, Greensboro na Roxboro ambayo imepata theluji inchi 8 na zaidi na imeripotiwa zaidi ya watu, 21,000 hawana umeme na ajali ni zaidi ya 260 zinazosadikiwa kusababishwa na theluji zimetokea usiku wa kuamkia jumamosi Jan 7, 2017. Watu wameombwa kukaa ndani kama huna ulazima wa kutoka sababu nje sio kuzuri na hali ya tahadhari ya theluji imetolewa kuanzia siku ya Ijumaa Jan 6 saa 1 jioni mpaka Jumamosi Jan 7, 2017 saa 1 jioni.
Hapa ni Harrsi teeter likiwa limejaa wateja wakijipatia mahitaji ya vitu mbalimbali siku ya ijumaa Jan 6, 2017 mji wa Durham.
Mji wa Winston-Salem mapema leo Jumamosi Jan 7, 2017.
Sehemu ya makazi mji wa Durham, North Carolina.
Hapa ni moja ya ajali iliyotokea Virginia ya kusini eneo linalopakana na North Calolina baada ya lori la mizigo kuteleza kutokana na theluji iliyokua imeanguka.
Hapa ni mji wa Raleigh siku ya Ijumaa jioni wakati wa rasharasha ya theluji.
Mtoto akiparua theluji katika mji wa Raleigh, NC.
0 comments:
Post a Comment