![]() |
Na Sosy
MKUU wa Mkoa
kijana kuliko wote mwenye ubunifu wa hali ya juu Paul Makonda ameweka mikakati
ya kuligeuza jiji hilo kuwa kama ulaya na muoenekana wa kisasa na kuwa mji wa
kuvutia zaidi. |
Moja yamipango yake ni kulifanya jiji hili kuwa safi ,kutenga maeneo ya biashara, usalama wa raia na mali zao, watumishi hewa, kurudisha hadhi ya watendaji wa Serikali za Mitaa, elimu na miundombinu bora, BLOG YA WANANCHI imeweza kuripoti.
Usafi; Makonda alitangaza zawadi ya
gari la Sh20 milioni au fedha taslimu kwa mwenyekiti ambaye mtaa wake utaongoza
kwa usafi na Sh5 milioni kwa kila mjumbe wa mtaa husika. Zawadi hiyo
itakayokuwa ikitolewa kila baada ya miezi mitatu, itaanza rasmi
Aprili Mosi
Ni kiongozi
mwenye falsafa ya kipekee katika uongozi ya kuamini maendeleo katika uchapakazi
na kwamba yeye hapendi nyakati za kufanya kazi kufanya siasa.
“Ninyi ni
kama viongozi wengine, nataka mtimize ahadi zenu mlizowaahidi wananchi kipindi
cha kampeni siyo kuleta siasa. Tushirikiane kuleta maendeleo katika jiji hili
linalotazamwa na kila mtu” hii nin kauli yake alipokuwa akizungumza na watendaji
559 wa mkao huo.
Maeneo maalumu ya biashara; Kiongozi huyu mbunifu anataka
mji wa Dar es Salaam kuuweka katika mazingira mazuri haswaa kwa kutenga maeneo
mazuri ya biashara ambapo wafanaya biashara watakuwa katika mazingira rafiki
kwa biashara zao pamoja na kuweka utaratibu nzuri wa kukusanya mapato.
“Ninatamani kuona Wilaya ya Kinondoni, Ilala na Temeke zikitenga
maeneo maalumu kwa ajili ya maduka ya magari na gereji pia.
Usalama; Makonda amekuwa makini katika
suala la usalama watu na mali zao kwa juhudi kubwa za kujenga vituo vya Polisi
vikubwa 20 katika jiji la Dar es Salaam ambalo awali lilikuwa lina matukio
mengi ya ujambazi.
Ametoa Motisha
kwa jeshi ya kutoa zawadi ya shilingi
milioni 1 kwa askari atakaye mtia nguvuni jambazi na waharifu wengine.
Amekuwa akiumizwa
roho akisikia matukio ya kikatilii yametokea ambapo tayari ameonekana
akidhihirisha kuchukizwa kwa matendo hayo kama alivyoendesha harambee ya
kumchangia kijana Saidi Mrisho aliyetolewa macho na Salum Nywete alimaarufu
Scopioni.
Elimu, Makonda yeye ni kijana msomi
anatambua umuhimu wa elimu na kwamba amekuwa mstari wa mbele kuchangia madawati
na ujenzi wa shule mbalimbali Mkoani Da es Salaam,
Pia aliwahikuwataka
watendaji na wenyeviti katika mitaa yao kutafuta wadau kusaidia sekta hiyo
badala ya kusubiri Serikali.
Miundombinu; tangu Makonda akabidhiwe Dar es Salaam tayari kuna mabadiliko katika ubora na wingi
wa miundombinu ikiwa pamoja na kupungua kwa foleni kero ya wananachi wa mji huu
ya foleni barabarani.
Wananchi wa
Dar es Salaam, wamebahatika kuongozwa na kiongozi kijana mwenye ubunifu wa hali
ya juu.
0 comments:
Post a Comment