
-Serikali itachangia ujenzi mara wananchi watakapoanza ujenziMkuu wa Mkoa wa Mbeya Amewataka watendaji wa Vijiji na kata KUHAMASISHA wananchi na wadau mbalimbali kuanza ujenzi wa zahanati kila kijiji na kituo cha Afya kwa kila Kata 

Hayo ameyasema leo wilayani chunya alipoongea na watendaji wa vijiji na kata na kuwakumbusha wajibu wao kama watendaji ni kutekeleza ilani YA Ccm kwa vitendo kwa kuhamasisha wananchi na wadau kuanza ujenzi wa zahanati kila kijiji na kituo cha Afya kila kata 

Amesema katika miaka mitano serikali kwa kushirikiana navwananchi lazima wajenge zahanati kila kijiji kisichokuwa zahanati na kila kata kituo cha afya kwa kata isiyo na kituo cha afya

Amehaidi yeye na wakuu wa wilaya watafuatilia utekelezaji wa ilani ya cm katika kila kijiji na Kata
Amewakumbusha watendaji kuwa serikali itaunga mkono wananchi pale watakapoanza ujenzi hivyo ni jukumu la watendaji kuwahamasisha wananchi kuanza ujenzi kwanza lengo ni kuwaounguzia umbali wananchi wetu kufuata huduma YA afya

0 comments:
Post a Comment