
MWALIMU Wiseman Ficky KUTOKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM..
Chini ujumbe wake kupitia mtandao wa facebook
Leo mada kubwa iyo break internet ni tukio la walimu wakioneka wanatoa adhabu kubwa sana kwa mwanafunzi.
Tukio hilo limepekea kila mtu ni lawama kwa walimu, walimu leo tumepokea matusi ya kila aina.
Nisema wazi mimi ni mwalimu kitaaluma. Ni mwalimu hasa wa kusomea
nilishapita shule na kufundisha miaka kadhaa kabla sijaamua kurudi zangu
tena chuoni ninaposoma hivi sasa.
Nikiri kwamba kitendo walichofanya hawa si chema, ni kitendo kibaya
lakini tunapolamu basi tuwe na staha. Tusifanye hii taaluma kuwa
chochoro kila mtu anapaswa kuisemea. Hebu mheshimu taaluma za watu. Nalaani vikali mkiotukana walimu humu
mitandaoni kuita walimu vilaza, washenzi, mashetani waliofeli, nk Haiingii akilini kosa la walimu wawili watatu likufanye kutukana walimu wote Tanzania.
Walimu ni watumishi na binadamu pia wanakosea wao si malaika, kama
ambavyo polisi hukosea kupiga raia, daktari hukosea kwa wagonjwa,
trafiki nao hukosea kudai rushwa, watumishi wengine mbali mbali hukosea
basi na hawa walimu nao wamekosea na wamefanya makosa lakini hatupaswi
kutukana walimu nchi nzima.
Narudia tena acheni matusi ya reja reja shenzi kabisa nyie kwanza
mnapata wa ujasiri wa kuwatukana walimu ambao hata wewe umepita mikononi
mwao?!
Je hakuona walimu wenye busara, wenye upendo waliojitolea kwa moyo wote kukufundisha mpaka ukajua kusoma na kuandika na ngazi zote za elimu hadi ukafika ahpo ulipo?!
Je hakuona walimu wenye busara, wenye upendo waliojitolea kwa moyo wote kukufundisha mpaka ukajua kusoma na kuandika na ngazi zote za elimu hadi ukafika ahpo ulipo?!
Waliokufundisha unawaita vilaza waliofeli? Mnazungumzia kufeli kupi?
Hivi kuna mwalimu div zero? Yani unashupaza kabisa shingo eti hakuna
mwalimu division one au division 2? Hebu njoo Leo Udsm faculty of
education ukikosa div one in two 1500+ njoo uropoke tena humu mtandaoni.
Niwapongeze wote walioamua kuangalia hili hili jambo kwa busara na kulaumu kwa busara bila kutukana walimu wao.
Taaluma ya elimu ya elimu nchini ina changamoto nyingi sana. Walimu wa
sasa wanakumbana na changamoto nyingi sana kuanzia katika mazingira yao
ya kazi hadi kwa wawanafunzi wanaowafundisha ieleweke sasa hivi jaami
iko hovyo kimaadili jambo linalopelekea baadhi ya watoto kuwa na nidhamu
mbovu.
Leo nipo serious kabisa.
Wapo vijana wamefikia hadi kupiga walimu wao, kuwatukana matusi ya nguoni. Imetokea wanafunzi kupiga mwalimu na kumtoa meno huko katavi cha ajabu sijaona reaction kama ya leo huku mitandaoni.
Wapo vijana wamefikia hadi kupiga walimu wao, kuwatukana matusi ya nguoni. Imetokea wanafunzi kupiga mwalimu na kumtoa meno huko katavi cha ajabu sijaona reaction kama ya leo huku mitandaoni.
Tufahamu kwamba shule nyingi serikali mwanafunzi hafukuzwi hata Mkuu wa
Shule hana uwezo wa kumfukuza mwanafunzi kwa maana ya kumtoa kabisa
shuleni jambo hilo limepeleka baadhi kutumia hiyo kama kigezo wanajua
wazi hawawezi kufukuzwa watakupiga itajadiliwa na itaisha.
Hebu leo hii wewe vaa viatu vya mwalimu aliepigwa mtama na mwanafunzi
wake mstarini, vaa viatu vya mwalimu alietolewa meno huko katavi. Vaa
viatu vya mwalimu anaeambiwa na mwanafunzi wake darasani hunibabaishi na
hunitishi wewe ni mjinga tu bila shaka ingekua ni wewe unayelamu humu
mitandaoni pengine ungefanya makubwa kuliko hata walimu wa kwenye ile
clip
Wapo wanafunzi ni wala bangi wazuri sana wao siku moja shule siku moja
road kuendesha boda boda. Ni manunda haswaa sasa walimu wamekua chaka la
walama baada ya jamii kuishindwa kuiweka sawa mitoto yenu huko nyumbani
mnaisukumia Shule walimu wahangaike nayo na ndio hii inayopiga walimu
na kuwakaba makoo kisa tu ameulizwa kwa nini hujaandika class work.
Walimu hawa vijana wako field bado hawajawa walimu kamili wapo masomoni
pengine mwaka wa kwwnza hawajamaliza bado kozi ya ualimu walikua hawana
uzoefu na changamoto za watoto minunda na ndio hizo wamekutana nazo na
kupelekea kushindwa kudhibiti hasira zao.
Walimu wakiwa bado jikoni hawajaiva wanapelekwa field wakakumbane na
mazingira halisi ya shule ili kuwajengea uwezo kamili sasa mbaya zaidi
mambo yamekua kama haya.
Wasalaam
Mwalimu kijana Wiseman Ficky
Imeandikwa na Wiseman Ficky
Imeandikwa na Wiseman Ficky
0 comments:
Post a Comment