Posted by Williammalecela.com on Friday, October 07, 2016
 |
Kijana Said Mrisho anayedaiwa kujeruhiwa na kutobolewa macho na Salumu
Henjelewe maarufu kama Scorpion (katikati), akisaidiwa na ndugu zake
wakati akiingia ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda
kuzungumza na waandishi wa habari.
|
 |
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia), akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari kabla ya kumpa fursa kijana Said
kuzungumza na wanahabari. |
 |
Kijana Said Mrisho (kulia), akizungumza na wanahabari. Kulia kwake ni mke wake Stara Soud. |
 |
Kijana Said Mrisho anayedaiwa kujeruhiwa na kutobolewa macho na Salumu
Henjelewe maarufu kama Scorpion (kulia), akilia kwa uchungu wakati
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mbele ya Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo. Kushoto ni mke wake, Stara Soud. |
 |
MAJONZI na vilio vilitawala ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda wakati Kijna Said Mrisho anayedaiwa kujeruhiwa na
kutobolewa macho na Salumu Henjelewe maarufu kama Scorpion Buguruni
Sheli alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mbele ya mkuu wa mkoa
Dar es Salaam leo asubuhi kuwa hata ona tena katika maisha yake
kufuatia kujeruhiwa vibaya kwenye mishipa ya macho na mtuhumiwa huyo na
kupoteza uwezekano wa kuona. |
 |
Mrisho alisema anamshukuru sana Rais John Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda kwa jitihada walizofanya za kumsaidia kupata
matibabu lakini imeshindika kwa kuwa mishipa yote yenye uwezo wa
kumfanya aweze kuona imeharibiwa vibaya na mtuhumiwa huyo hivyo ataweza
kuona tena katika maisha yake."Iwapo kama mishipa isingeharibiwa kwa visu mama yangu kipenzi Halima
Lwiza Abdallah alikuwa yupo tayari kutoa jicho lake moja kwa ajili ya
kunisaidia niweze kuona lakini kwa bahati mbaya hilo halitawezekana
baada ya madaktari kunieleza kuwa mishipa ya macho yangu imeharibiwa"
alisema Mrisho kwa huzuni na kuanza kulia.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wamepokea kwa huzuni
taarifa hiyo ya madaktari na kumuomba Mrisho asikate tamaa kwani
serikali itaangalia jinsi ya kumsaidia.Makonda alisema serikali itatoa sh.milioni 10 kama mtaji ili ziweze
kumsaidia wakati wakiangalia namna ya kuwashirikisha watu
wengine kwa ajili ya kumsaidiaMakonda alisema serikali itamsaidia kufanyiwa upasuaji wa kuwekewa macho
ya bandia ili awe katika mwonekano wa kawaida ingawa hatakuwa haoni."Pamoja na kumpatia kiasi hicho cha fedha katika kipindi hiki cha mpito
ambacho atakuwa akihitaji kwenda katika matibabu na sehemu zingine
tutakuwa tukimsaidia usafari wa kwenda maeneo hayo" alisema Makonda. |
 |
Said Mrisho akisaidiwa kushuka ngazi wakati akitoka kuzungumza na wanahabari ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam |
"Nilijua ipo siku moja nitakufa lakini sikutegemea kuwa nitakuja
kutolewa macho yangu kikatili kiasi hiki sijui mungu anampango gani na
mimi wala sijui nini ya hatima ya maisha yangu" alisema Mrisho ambapo
ukumbi mzima uligubikwa na ukimya sanjari simanzi huku mke
wake Stara Soud akishindwa kujizuia kulia.
0 comments:
Post a Comment