Posted by Williammalecela.com on Wednesday, September 14, 2016
Ntaganda analaumiwa kwa kuwatumia watoto kama wanajeshi, na wanake kama watumwa wa ngono
Kamanda wa zamani
waasi nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, ambaye anakabiliwa na kesi
katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC huko Hague,
amasema kuwa yuko tayari kufa badala ya kuvumilia hali anayopitia kwa
sasa akiwa kizuizini kwa mujibu wa shirika la habari ya Reuters.
Bosco
Ntaganda ambaye analaumiwa kwa kuwatumia watoto kama wanajeshi, na
wanawake kama watumwa wa ngono na pia mauaji nchini Jamhuri ya
Demokrasia Congo kati ya mwaka 2002 na 2003, alianza mgomo wa kutokula
chakula wiki iliyopita.
Ntaganda anasema hana uwezo wa kumuona mkewe na watoto
"Sina uwezo wa kumuona mke wangu na watoto tena
katika hali nilivyo sasa. Hii ndiyo sababu imenifanya nipoteze
matumani.Ndiyo sababu niko tayari kufa," Ntaganda alisema katika taarifa
iliyosomwa na wakili wake. Ntaganda alikana mashtaka yote 18 dhidi yake wakati wa kuanza kwa kesi mwaka uliopita.
0 comments:
Post a Comment