Taarifa
zilizopo kwa wengi ni kuwa Chidbenz amerudi tena kutumia Dawa za
kulevya hata baada ya msaada kutoka kwa DiamondPlatnumz na ungozi wake
kumpeleka Reharb.
Kwa mujibu wa Dulla mtangazaji wa PB amesema chid benz amekana shutuma hizo na kusema si kweli kuwa amerudi tena kutumia dawa.
Kupitia
PB Dulla amesema alikutana na chidbenz wakiwa kwenye maongezi ya
kawaida akamuliza kuhusu kinachosemwa mtaani chid akalalamika sana
kuhusu story hizo ambazo hata yeye alisema anazisikia ila si za kweli.
Kuna
matukio kadhaa yamekuwa yakiripotiwa na watu mfano ujumbe mmoja
uliosambaa mitandaoni ukisema chid kaonekana Nyumba moja ya kulala
wageni akionekana kulewa huku akimfanyia fujo msichana aliyekuwa
naye(jina halikutajwa).
Tukio la pili anadaiwa ameonekana akibebwa na
watu huku wengine wakimzomea kwa kitendo chake cha kuonekana amelewa
baada ya kutumia Unga.
Hata hivyo hakuna uthibitisho wa kujiridhisha kuhusu matukio hayo.
Chiku
keto mmoja wa wasanii waliokuwa chini ya chid (LaFamilia)alipoulizwa
ameonekana kutokuwa na ukaribu na chid na amesema walikubaliana kupeana
sapoti lakini yalikuwa maneno tu hakuna kilichoendelea.
Mwanzoni Chid
alikuwa anaonekana sana akiwa na wasanii wa Lebo ya Wcb lakini baada ya
kutoa ngoma yake Chuma yupo kivyake.hata hivyo juzi kati alikuwa na
show mkoani Dodoma.
0 comments:
Post a Comment