
Mwanadada
anayeuza sura kwenye video mbalimbali za wasanii wa Bongo Fleva, Gift
Stanford ‘Gigy Money’ ameibuka na kusema kuwa kitendo cha Mwanamuziki
Esterlina Sanga ‘Linah’ kuamua kumchukua mpenzi wake, Idris Sultan ni
dhahiri kwamba anafanya malipizi hivyo kamwe hatamvumilia.

Mwanamuziki Esterlina Sanga ‘Linah’
Akichonga
Gigy Money ambaye awali aliingia kwenye vita ya maneno na Mwigizaji
Wema Sepetu baada ya kumkwapulia bwana (Idris), alisema Linah amelipiza
kisasi kwa kuwa aliwahi kumchukulia mpenzi wake, Billnas ila anafanya
juu chini mpaka amrudishe Idris kwenye himaya yake.

Mwanamuziki Esterlina Sanga ‘Linah’
“Linah
ameamua kulipa kisasi baada ya mimi kutembea na aliyekuwa mpenzi wake,
Billnas ambaye niliona hajui mapenzi nikaamua kumpiga chini, sasa huu
moto ndiyo umewaka, yule hawezi kushindana na mimi, anisikilizie tu
atajua mimi ni nani kwanza Idris lazima nimrudishe kwenye himaya yangu,”
alisema Gigy Money.

Gift Stanford ‘Gigy Money’
Baada
ya Gigy kuweka wazi hayo, gazeti hili lilimtafuta Linah ili kujibu
tuhuma hizo lakini simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa
ujumbe mfupi wa maneno kwenye Mtandao wa Kijamii wa WhatsApp hakujibu
chochote licha ya kuonesha kwamba ameusoma.
0 comments:
Post a Comment