Posted by Williammalecela.com on Monday, September 19, 2016
|

|
Kesi dhidi ya wanawake watatu
walioshukiwa kuhusika katika shambulio dhidi ya kituo kimoja cha polisi
katika mji wa bandarini wa Mombasa nchini Kenya mwishoni mwa juma,
ilishindwa kufanyika kutokana na matatizo ya mawasiliano.
Mmoja wa washukiwa hafahamu kabisa Kiingereza au Kiswahili.
Shukri
Ali, ambaye ni mlemavu wa kutosikia, hakujibu lolote hata baada ya
mfasiri wa ishara aliyeletwa mahakamani kumsaidia kuelewa kesi dhidi
yake.
Mtafsiri wa lugha ya Kisomali pia alikuwa mahakamani ili
kuwasaidia washukiwa wawili, Saida Ali na Naima Mohamed Ali, ambao
hawana uwezo wa kufahamu Kiingereza. |
 |
Shukri Ali, Saida Ali na Naima Mohamed Ali mahakamani, Mombasa
|
Jaji Emmanuel Mutunga, aliamuru Shukri Ali, kupelekwa hadi katika
wachunguzi maalum wa kimatibabu, katika hospitali ya kitaifa ya Coast
General. Wanawake hao watatu, ambao bado wanazuiliwa pia watachunguzwa na madaktari. Wanashtakiwa
kwa kosa la kuwapa hifadhi wanawake watatu wanaodaiwa kuunga mkono
kundi la Islamic State, ambao waliuwawa pale walipojaribu kushambulia
kituo cyha polisi cha Mombasa siku ya Jumapili iliyopita.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 21, wakati ripoti ya kimatibabu itakapowasilishwa mahakamani. |
0 comments:
Post a Comment