![]() |
| Diamond Akiwa na Mpenzi wake Zari Hassan |
Hakuna baraka za muhimu kuzipata kama zile za mzazi wako na zile za mtu umpendaye.
Kwa
mwanaume baraka kutoka kwa mke wake zina nguvu mno hasa kwakuwa
maandiko matakatifu yanasema kuwa mwanamke alitokana na ubavu wa
mwanaume. Mrs Nasib Abdul, Zari amempa baraka zake mpenzi wake Diamond
ambaye amesafiri kwenda Los Angeles, Marekani kwenye tuzo za BET.
Diamond ametajwa kuwania kipengele cha Best International Act: Africa.
“Safari
njema. May the Good Lord be with you all the way. Praying you bring the
BET Award back to East Africa…. xoxo😍 @diamondplatnumz,” ameandika
Zari kwenye Instagram.
Hata
hivyo kipengele hicho kina upinzani mkubwa mwaka huu. Msanii pekee
ambaye ni tishio kwa Mond ni Wizkid. Staa huyo wa Nigeria mwaka huu
amefanya mambo makubwa ikiwemo kushirikishwa na Drake kwenye wimbo ‘One
Dance’ ulioshika nafasi ya kwanza kwenye Billboard Hot 100 kwa wiki sita
mfululizo. Pia amezunguka na Chris Brown kwenye ziara yake ya One Hell
of A Nite’ barani Ulaya.
Wasanii wengine wanaowania kipengele hicho ni AKA, Cassper Nyovest, Yemi Alade na wengine.

0 comments:
Post a Comment