Na mwandishi wetu
WAKATI
Waislam wakiwa kwenye Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, staa wa
filamu Bongo, Irene Uwoya juzikati alimtia majaribuni msanii mwenzake
Single Mtambalike ‘Richie’ walipokuwa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee
jijini Dar kulikokuwa na harusi ya mdogo wake Steve Mengere ‘Steve
Nyerere’, Happy Mengere.
Kwenye
‘mnuso’ huo, Uwoya aliyekuwa amevalia kivazi kilichoacha mapaja yake
wazi, alionekana mara kadhaa akimkumbatia Richie na hata paparazi wetu
alipotaka kuwafutoa picha, staa huyo alimshika kimahaba na kuwaacha watu
wakinong’ona chinichini.
“Uwoya
hivi haoni anamtia mwenzake majaribuni? Na Mwezi Mtukufu huu
analazimisha kupiga naye picha ya kumkumbatia, ila hawa wasanii
wamezoeana sana,” alisema mmoja wa waalikwa aliyekuwa karibu na mastaa.
Paparazi
wetu aliyekuwa eneo la tukio alipojaribu kuwakaribia na kumuuliza Uwoya
kulikoni anamfanyia mwenzake vituko alisema, alijisahau kuwa Richie
yupo kwenye Mwezi Mtukufu ila alipiga picha hiyo kama pozi la kawaida tu
na wala hakuwa na nia mbaya.
0 comments:
Post a Comment