,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, June 24, 2016

Irene_Uwoya028
WAKATI Waislam wakiwa kwenye Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, staa wa filamu Bongo, Irene Uwoya juzikati alimtia majaribuni msanii mwenzake Single Mtambalike ‘Richie’ walipokuwa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar kulikokuwa na harusi ya mdogo wake Steve Mengere ‘Steve Nyerere’, Happy Mengere.

uwoya richie (1)
Irene Uwoya na Richie.

Kwenye ‘mnuso’ huo, Uwoya aliyekuwa amevalia kivazi kilichoacha mapaja yake wazi, alionekana mara kadhaa akimkumbatia Richie na hata paparazi wetu alipotaka kuwafutoa picha, staa huyo alimshika kimahaba na kuwaacha watu wakinong’ona chinichini
uwoya richie (2)
Single Mtambalike ‘Richie’
“Uwoya hivi haoni anamtia mwenzake majaribuni? Na Mwezi Mtukufu huu analazimisha kupiga naye picha ya kumkumbatia, ila hawa wasanii  wamezoeana sana,” alisema mmoja wa waalikwa aliyekuwa karibu na mastaa.
Paparazi wetu aliyekuwa eneo la tukio alipojaribu kuwakaribia na kumuuliza Uwoya kulikoni anamfanyia mwenzake vituko alisema, alijisahau kuwa Richie yupo kwenye Mwezi Mtukufu ila alipiga picha hiyo kama pozi la kawaida tu na wala hakuwa na nia mbaya.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi