Huku kukiwa na madai ya ndoa ya
staa wa Bongo Fleva, Hamis Ramadhan ‘H. Baba’ na mwigizaji Flora Mvungi
kusambaratika, mwana mama huyo amedaiwa kurudi nyumbani kwa mama yake
mzazi, Kimara jijini Dar.
Awali, mtoa taarifa wetu ambaye ni mtu
wa karibu na familia hiyo, amedokeza kuwa chanzo cha Flora kurudi kwao
Kimara ni mzozo uliotokea katika hoteli moja iliyopo Magomeni Mwembechai
(jina linahifadhiwa).
“Mzozo ulikuwa mkubwa siyo kitoto,
mastaa wote wanajua, wanajitahidi kuwasuluhisha ili suala lisifike
magazetini. Flora alitoa picha zote za mumewe, lakini mama (anatajwa
jina mdau mkubwa wa filamu, ambaye hakupatikana) akamshauri arudishe
picha hizo ili watu wasishtukie, ndo anaweka kwa shingo upande lakini
kwa sasa Flora yupo nyumbani kwao Kimara na H. Baba ametimkia Mwanza,”
kilisema chanzo hicho.
Alipotafutwa H. Baba kwa njia ya simu, alikiri kuwa yupo Mwanza na mkewe yupo kwao Kimara lakini hakuna mzozo wowote kati yao.
Alisema hashangazwi na habari hizo kwa
sababu siku zote watu wamekuwa wakimuombea mabaya katika ndoa yake,
kwanza walianza hivyo tangu walipooana wakidai wasingeweza kufikisha
mwaka mmoja wakiwa pamoja.
“Kuna watu wanatuombea mabaya tangu
zamani, sisi tupo imara na hakuna wa kututenganisha isipokuwa Mwenyezi
Mungu,” alisema H. Baba na kuongeza kuwa;
“Mke wangu kweli yupo kwao kwa sababu
kila nikisafiri yeye huenda huko ambapo hukaa wiki au zaidi na
ninaporudi naye hurejea. Ameenda na watoto wote na kule nyumbani kwangu
wapo wadogo zangu.”

0 comments:
Post a Comment