,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, June 17, 2016

 

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla amewataka wafanyabiashara wakubwa wa sukari mkoani Mbeya kusambaza kwa kasi sukari wanayoipata ili katika halmashauri zote mkoani Mbeya kusiwepo na upungufu wa sukari 
Hayo ameyasema leo katika kikao cha pamoja kati ya wafanyabiashara wakubwa wa sukari , bodi ya sukari na maafisa biashara na kuwaeleza kuwa mkoa katika wiki ijayo utapokea sukari toka Malawi tani 2000 na tangu alipotangaza kuingia kwa tani 1000 wiki iliyopita upatikanaji wa sukari umeongezeka na bei imeanza kushuka
Amewataka wafanyabiashara hao kushushwa bei ya sukari kadri sukari inavyongezeka katika soko na amewaeleza kuwa viwanda vya ndani vimeanza uzalishaji na wakati wowote kuanzia kesho tutaanza kupokea sukari toka viwanda vyetu vya ndani hivyo ni mategemeo ya serikali kuona bei ya sukari inashuka zaidi
Kwa mujibu wa maelezo ya wafanyabiashara wa sukari ni kwamba bei ya sukari imeanza kushuka wao sasa bei ya jumla wanauza kili sh 2,050 na rejareja wanauza kati ya sh 2.200 hadi 2,300 ila wanaamini kwa kuingia tani 2000 wiki ijayo na sukari toka kilombero bei ya sukari itashuka zaidi

 

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi