IMELDA MTEMA, Amani
Dar
es Salaam: Familia ya Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiwemo mama yake
mzazi, dada zake watatu na mdogo wake, wamenusurika kupoteza maisha
baada ya gari walilokuwa wakisafiria, kupata ajali mbaya kwenye makutano
ya Barabara za Ali Hassan Mwinyi na ile ielekeayo kwenye Ufukwe wa
Coco, Amani linakujuza.
Akizungumza
kwa masikitiko, Hoyce alisema ajali hiyo ilitokea mchana wa Jumapili
iliyopita wakati wanafamilia hao wakielekea Ufukwe wa Coco kwa ajili ya
kupata chakula cha mchana ambapo ghafla, gari jingine aina ya Range
Rover Vogue, lililigonga gari walilokuwemo ndugu zake na kuwasababishia
madhara makubwa.
Hoyce
aliongeza kuwa alipata taarifa za kupata ajali ndugu zake hao wakati
akiwa Bagamoyo, Pwani kwenye kambi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi.
Mama mzazi wa Hoyce Temu
Mrembo
huyo alisema kuwa alipigiwa simu na dada yake mkubwa aitwaye Edith
aliyekuwa kwenye ajali hiyo na kumtaarifu kwamba wamepata ajali mbaya na
hali ya mama yao siyo nzuri, jambo lililomlazimu kurejea haraka jijini
Dar es Salaam hadi Hospitali ya Taifa Muhimbili walikokuwa wamelazwa.
Kwa
mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo ilitokea baada ya kijana mwenye asili
ya Kisomali, aliyekuwa akiendesha Vogue, kuvunja sheria za barabarani
kwa kuendesha kwa mwendo kasi na kusababisha aligonge gari hilo,
lililokuwa likiendeshwa na mdogo wa Hoyce aitwaye Rachel.
Baada
ya kufikishwa Muhimbili, majeruhi wote walipatiwa matibabu ya awali na
kulazwa kwenye Wodi ya Kibasila ambapo wawili waliruhusiwa kutoka na
wengine wawili, akiwemo mama yake mzazi, walibaki hospitali.
“Kwa
kweli ilikuwa ni ajali mbaya sana, namshukuru Mungu kwani ningepoteza
familia yangu yote na hapa bado namuuguza mama yangu na ndugu zangu
ingawa wengine wanae-ndelea vizuri,” alisema Hoyce.
0 comments:
Post a Comment