Posted by Williammalecela.com on Wednesday, June 15, 2016
Mkuu wa MKOA wa Mbeya Amos Makalla ametengua AMRI ya kuvifungia viwanda
vidogo 28 vya kukoboa mpunga eneo la Sido iliyotolewa na jiji la Mbeya
kupitia idara ya mazingira sababu ya kuvifungia viwanda hivyo zikielezwa
kuwa ni mlundikano wa pumba katika maeneo hayo Uamuzi wa kutengua
amri hiyo ametoa leo kwenye ziara ya kutembelea ofisi ya Sido Mkoa na
kisha kutembelea karakana ya sido, viwanda vidogo vya uzindikaji na
ukamuaji mafuta ya alizeti na viwanda vya kukoboa mipunga eneo la sido
na hapo ndipo alipokutana na umati wa wananchi wakiomba msaada wake
kwakuwa viwanda hivyo vimebeba ajira ya watu zaidi ya 2000 Baada ya
kuwasikiliza wananchi hao alitangaza kutengua amri hiyo kwa kuwa
kuvifunga viwanda hivyo kutafanya mchele kuadimika na bei itapanda na si
jambo jema hasa kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu Pili
ametengua amri hiyo ikizingatia kuna ajira zaidi ya watu 2000 . "Kwa
amri hii ya kufunga ukoboaji hivi Hawa watu 2000 wanakwenda wapi? Kama
si kurudi mtaani na kwa vijana ni hatari. Hii kauli ya hapa kazi tu kwa
Hawa watu 2000 wataifanyia wapi?" Ameagiza Mkuu wa wilaya, jiji ,
jumuiya ya wakoboaji washirikiane na uongozi wa Mbeya cement ambao ndiyo
watumiaji wa pumba hizo kuongeza uwezo wa kusomba pumba hizo Akiwa
eneo la Sido magari ya Mbeya cement yaliendelea kusomba pumba na
wamemuhaidi Mkuu wa mkoa ndani ya wiki mbili pumba zote zitakuwa
zimesombwa
0 comments:
Post a Comment