v
Zaidi ya magari 40 yaanza safari ya kupeleka huduma mikoa yote nchini
v
Gulio kubwa kufanyika Mlimani city kuanzia kesho mpaka jumapili
Katika
kutekeleza agizo la Mamlaka ya Mawasiliano nchini(TCRA)la kuzitaka
kampuni za mawasiliano kutoa elimu kwa wateja wao kuhusiana na simu
zisizokuwa na kiwango
yaani simu feki,Vodacom Tanzania leo imezindua kampeni maalum ya
uhamasishaji wa huduma zake mbalimbali ikiwemo kusajili laini za wateja
kwa njia ya kieletronikali pia kuwauzia wateja simu halisi na za gharama
nafuu.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa bidhaa za Vodacom,Hassan Saleh
amesema kuwa lengo ya kampeni hii itakayofanyika kwenye mikoa yote ya
nchi,mijini na
vijijini ni kutoa elimu na kutangaza matumizi ya huduma mbalimbali za
Vodacom pia kuwapelekea bidhaa bora za mawasiliano na za gharama nafuu.
“Kipindi
hiki ambacho simu feki zinazimwa tumeona ni vema tuwafikie wananchi
hususani wanaoishi maeneo ya vijijini na kuwauzia simu halisi na za
gharama nafuu
ili wasiachwe nje ya mawasiliano,pia tutasajili laini za wateja ambao
walikuwa wanatumia simu bila usajili ili kuwaepusha kuangukia kwenye
mkono wa sheria kwa kufanya hivyo vile vile tutawaelimisha jinsi ya
kunufaika na huduma zetu mbalilmbali hususani huduma
ya kukopa kwa kutumia simu ya mkononi ya M-Pawa bila kusahau huduma ya
M-Pesa”.Alisema
Saleh
alisema hii sio mara ya kwanza kampuni kuwafuata wateja imekuwa
ikifanya hivyo mara kwa mara kwa kuwa inaamini kuwa wateja ndio namba
moja katika biashara
zote inazofanya “Kwetu wateja wetu ni wafalme,tanawapenda,tunawajali na
kuwasikiliza ndio maana tumeona kuna umuhimu wa kuwafuata popote walipo
na kuwaelimisha ni kwa jinsi gani watanufaika na huduma zetu na
kuboresha maisha yao ikiwemo kuwapatia zawadi mbalimbali
bila kusahau burudani zinazoenda sambamba na kampeni hii”.Alisema
Kuhusiana
na huduma ya M-Pawa inaowawezesha wateja kujipatia mikopo kupitia simu
zao za mkononi alisema huduma hii imeanza kupata mafanikio makubwa
“"Kadri siku
zinavyozidi kusonga mbele ndivyo wananchi wengi wamekuwa wakizidi
kuelewa huduma hii mpya zaidi ya matarajio yetu na watu wengi wamefungua
akaunti na wengine wanazidi kujiunga kila kukicha na wengi tayari
wameanza kupata mikopo kupitia huduma hii.Mpaka sasa
zaidi ya watanzania milioni moja wanatumia huduma hii”.Alisema.
Alisema
teknolojia hii ya M-Pawa au “kibubu” ni mkombozi kwa wananchi wengi wa
Tanzania ambao walikuwa hawajafungua akaunti za benki “Kuna wananchi
wengi wamekuwa
na utaratibu wa kukaa na fedha nje ya mabenki,ambako hazileti riba
zinawekwa kwenye magodoro,wengine kuzichimbia ardhini na darini,fedha
hizi haziko salama ni bora kuziweka M-Pawa”anasema Saleh.
Aliwataka
watanzania kuchangamkia fursa hii kusajili laini za simu zao,kununua
simu halisi na vifaa vingine vya mawasiliano bila kusahau kufika katika
gulio kubwa
na la aina yake hapo kesho katika makao makuu ya kampuni hiyo kuanzia
saa 4 asubuhi.Alisisitiza.
Mwisho
|
0 comments:
Post a Comment