![]() | |
Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe (Picha kutoka Maktaba) |
Siku chache baada ya kuteuliwa na Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli kuweza kuongoza Wizara ya Maliasili na Utalii. Waziri mwenye dhamana ya kuongoza wizara hiyo Profesa Jumanne Maghembe Ameanza kwenda na Kasi ya Magufuli inayotambulika Duniani kote kama "HAPA KAZI TU"
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa
Jumanne Maghembe, amesema kipaumbele chake kikubwa kitakuwa ni kupambana
na ujangili nchini.
“Niwaambie majangili sasa
wakafanye kazi nyingine ama wakae nyumbani, kiama kinakuja huko, jambo
la pili nitakaloshughulikia ni misitu, kuitunza na kupambana na
usafirishaji wa magogo na ukataji wa mkaa,” alisema Profesa Maghembe.
Alisema kuwa atasimamia kwa uhakika
maliasili za Watanzania kwa sababu mambo ya maliasili ndiyo eneo
alilobobea kwenye usomi wake.
“Tutajitahidi pia kutangaza
utalii na kuongeza mapato ya sekta hii kama tulivyofanya kwenye miaka ya
2006 hadi 2008, tuliongeza bei za vitalu na ada kwa mnyama mmoja mmoja
anayewindwa,” alisema Profesa Maghembe.
0 comments:
Post a Comment